Huna Sababu Ya Kutoanzisha Blogu LEO! Jambo Usilofahamu Kuhusu Millard Ayo

Kama unamiliki (una mpango) blogu na unaitumia kujenga biashara yako lakini hupati matokeo uliyokusudia basi hakikisha unatia umakini katika maneno yafuatayo.

Ninachoenda kukushirikisha katika makala hii ni stratejia zinazotumiwa na wana masoko wa mtandaoni walio kubuhu (online marketing gurus), kunasa mamia ya wateja kwa siku, kufanya mauzo na kuingiza mamilioni ya pesa katika akaunti zao…

…Kwa Kasi Ya Mwanga!

….Wanatumia Blogu Kama Nyenzo Kuu Muhimu Kufanikisha Azma Yao!

Kabla sijaeleza ni kwa namna gani, ni vema nianze na tafsiri…

Ni Nini Maana ya Blogu?

Blogu ni kurasa ama vitabu vya kuandika mambo ya kibinafsi kwenye Intaneti.

Swali ni Je…

Kwa nini zinavutia? Blogu hupa mtu nafasi ya kuandika mawazo yake, mapendezi na mambo anayofanya. Blogu nyingi zinawaruhusu wasomaji waandike maelezo yao na watu wengi wanafurahi wanapopata kwamba mtu fulani ameandika maelezo yake.

Unachopaswa kujua ni kwamba, habari zilizo kwenye blogu zinaweza kusomwa na mtu yeyote.

Kwa wana masoko, wao blogu ni zaidi ya maelezo ya kiujumla niliyotoa hapo juu.

Kwao, blogu ni dhana ambayo huitumia kupeleka ujumbe kwa watu maalumu (walengwa) kuwapa taarifa au elimu inayokusudia kuwajengea mamlaka machoni kwao huku wakitakiwa kuchukua hatua zaidi (kuboresha mahusiano, kufanya mauzo n.k). Chochote utakacho chapisha hakikisha kinaweza kusambazwa, kuchangiwa, kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa Nini Kumiliki Blogu Ni Muhimu Katika Biashara Yako?

Kwa maana umuhimu wa kutambulika kwa biashara yako machoni pa watu ni wa kiwango cha juu na muhimu kwa ufanisi wa biashara yako, hivyo kuwa na media mtandaoni mfano blogu inaweza kuwa ni dhana nzuri kwako.

Blogu yako itakuwa ikiongea, kusimulia na hata kukusaidia kufanya mauzo kwa niaba yako. Na kila ujumbe utakaochapisha kwenye blogu yako yawezekana kabisha ukasomwa na mamia na hata maelfu ya watu katika muda wao. Jambo linalokupa unafuu wa kukutana na watu wengi sana huku ukitumia nguvu chache mno ambazo haziwezi kufikiwa na mtu anayetumia njia za kizamani zilizo zoeleka.

Hebu nikupe mfano halisi… huwa napata wastani wa watembeleaji takribani 500+ kwa siku katika blogu ya Lusabara.com kwa mujibu wa Google Analytics. Nyingi ya makala zangu husomwa na watu zaidi ya 1000+.

Hii ina maana gani?

Kwa lugha nyingine, ina maana kwamba ilinibidi niwakusanye hao watu 1000+ mahala pamoja ili niweze kuwaambia kile kilichokiandika hapa. Je, ni kazi rahisi kuwakusanya watu 1000+ katika eneo moja kwa wakati mmoja? Kama jibu ni NDIYO, je, ni gharama kiasi gani zitatumika kuwafikishia taarifa na kuandaa ukumbi wenye kumudu kiwango hicho? Usipopata jibu, waulize waandaaji wa sherehe na mikutano…watakueleza!

Kama hujaelewa mfano huo, hebu nikupe mwingine wa kijana mtanzania ninayeamini anatengeneza kiwango kikubwa cha pesa kupitia mtandao.

ONYO!
Usiendelee Mbele Kama Wewe Ni Mmiliki wa Chombo Cha Habari.
Waweza Jikuta Unakatia Tamaa Biashara Yako.
La Sivyo, Uwe Tayari Kukubaliana Na Ukweli Huu!

Kijana Millard Ayo. (Naomba nikiri hapa kwamba sikuwahi kukutana naye uso, hivyo unachokisoma hapa hapa ni mtizamo wangu wa jumla katika industry). Tuendelee…

Hebu tizama Video hii hadi mwisho utagundua jambo… (ukitoka kapa nitakueleza japo kwa ufupi hapo chini)

Katika mahojiano hata wewe yawezekana unafikiri kwamba ni kwa ajili ya kukufurahisha kwa kuangazia maisha ya Jokate, la hasha… Ninaamini, kwanza waandaaji wa Miss Tanzania waliamua kumpa kazi Joketi ya kuwa msemaji wao wakilenga mbali zaidi (…to gain popularity at zero cost). Na katika mahojiano ya katika video hii naamini Millard Ayo katengeneza hela nzuri. Kama hakufanya hivyo basi wampeleke Milembe akatibiwe, 🙂 🙂 (Natania…)

Ni kweli… akatibiwe kama hajatengeneza hela kubwa hapo. Kipande cha picha hapa chini kinaakisi mtizamo wangu juu ya video hiyo. Hivi ni chombo gani hapa chini kinaweza kuteka hisia za watu zaidi ya 200K kwa zaidi ya dakika 10 wakitizama tangazo? Kwa walio wengi, wakati wa matangazo (hata la dakika 1) wao hubadili chaneli. Ni wangapi wanaweza wakatizama tangazo kwa zaidi ya dakika 10? Wachache sana…

Hebu ona… Watazamaji 210,643!!

 

 

 

 

 

Jambo lingine ambalo huenda ulijui kuhusu Millard Ayo ni hili hapa: Ana wafuasi zaidi ya 2,771,234 huku akiwa ame-post mara 16,566!

Sina hakika kama yeye anajua utajiri alio nao kwa sababu hiyo, lakini kwa wale wataalam wa masoko wanaelewa namaanisha nini hapo. (Nitaeleza katika makala za usoni).

Hivyo ndivyo intaneti ilivyo biashara kubwa inayosadikika kuua vyombo vingi vya habari ulimwenguni. Ninavionea sana huruma hususani vituo vya redio na televisheni vyenye milengo fulani fulani ya kisiasa, itikadi, imani… visivyoaandaa vipindi vya uchambuzi, vitafungwa hivi karibuni kwa maana havitakuwa na wasikilizaji/watazamaji. Kitendo hicho kitavikosesha vituo hivyo kupata matangazo na hivyo vitashindwa kujiendesha.

Hebu nisaidie, ni kituo gani cha TV/Redio kwa sasa kinakuwa na watazamaji/wasikilizaji zaidi ya 200,000 kwa wakati mmoja? Kwa lugha nyingine, ni mfanyabishara yupi atakayependelea kutangaza na kituo cha habari kwa gharama kubwa huku tangazo lake likiwafikia idadi ndogo ya watu? Labda kama alikula mafuta ya mwenge 🙂 … Kwa nini usiende kwa Millard ukafanya naye kipindi kwa gharama ndogo na ujumbe wako ukawafikia watu wengi?

Ndo maana ya kutoa taadhari kwa wamiliki wa vyombo vya habari kutoisoma makala haya. Katika makala zijazo, nitajadili kitakwimu namna Faceboo na YouTube LiveStream zinavyokuja kubadili upepo wa Televisheni na namna unavyoweza kuanza kunufaika!

Mwenye masikio ya kusikia, utakuwa umenisikia!

Sasa hebu tuone…
Ni Kwa Namna Gani Unaweza Kutengeneza Pesa Kutumia Blogu Yako.

Ili uweze kutengeneza pesa kutumia blogu yafaa uwe na haya yafuatayo:

  1. Miliki blogu yenye kuvutia ( kama hii) 🙂
  2. Lenga watu sahihi
  3. Chapisha makala nzuri
  4. Nasa wateja (jenga orodha yao)
  5. Jenga mahusiano mema na orodha yako,
  6. Ingiza hela kila kukicha

1: Miliki blogu yenye kuvutia.

Kama wewe si mtaalamu wa kusanifu tovuti basi yafaa utafute designer mzuri wa kukutengenezea blogu yako ndani ya muda mfupi ikiwezekana. Huna la kusubiri. JEMAYA InfoSystems wanaweza kukusaidia katika hilo.
2: Lenga Watu Sahihi
Kama umekuwepo katika biashara kwa muda mrefu sasa, bila shaka umekuwa ukiambiwa kuwa “biashara yako ni kila mtu na kila mmoja.” Ki-halisia, nachelea kukueleza kuwa uko mbali na ukweli wenyewe. Biashara yako SI ya kila mtu na hata kila mmoja. Kama unafanya biashara yako huku ukiwa na mtizamo huo, huna tofauti na mtu anayejaribu kuuza kitimoto karibu na msikiti. Kama unataka kutengeza pesa, huna budi kufahamu kundi la watu sahihi wa bidhaa na hata huduma ya biashara yako. Inabidi ulenge kundi la watu wanaohitaji bidhaa na huduma yako. Huitaji kushawishi mtu anunue bidhaa yako. Huo ni umachinga na hali hii tunaiona sana sana kwa watu wanaofanya biashara ya mtandao (Network Marketing). Nitawazungumzia kwa undani zaidi katika makala zijazo…

Lenga kundi la wateja wako, wafahamu vizuri…andika makala inayolenga kuwazungumzia undani wa changamoto zao na namna ya kuondokana nazo. Kwa mfano, nimeandika makala hii kuwalenga watu wanaitaji kujenga biashara zao wakiwa nyumbani kwa kutumia laptop hata kama hawana ujuzi wa masuala ya kompyuta. Dira yangu ni kupunguza ombwe la watu wanaopata kadha za ajira hapa nchini.

3: Chapisha Makala Nzuri
Sababu namba moja ya ni kwa nini wafanyabishara wengi hawatengenezi pesa kupitia blogu zao ni kwa sababu wanatumia blogu zao kutangaza bidhaa na hata huduma zao. Nakushauri wewe usifanye hivyo, badala yake fuata ushauri huu wa Bw. Perry Marshal:

“Anybody who bought a drill, never wanted to buy a drill.
They wanted to make holes.
If you want to sell drills, do not advertise information about drills.
Advertise information about making holes.”

Kwamba (Tafsiri isiyo rasmi):

“Yeyote anaye nunua mashini ya kutoboa matundu, huwa hanunui mashini.
Anachohitaji ni kutoboa matundu.
Endapo unataka kuuza hizo mashini, usitangaze taarifa kuhusu mashini, badala yake…
Tangaza habari kuhusu utoboaji wa matundu.”

Kama wewe unafanya biashara ya nguo na ungependa kutumia blogu yako kujenga biashara yako hiyo, usiweke picha yoyote ya nguo kwenye blogu na hata usijaribu kuuza nguo kupitia blogu yako… badala yake anza kuandika makala kuhusu mwonekano. Kwa maana kila anayenunua nguo nzuri, huwa afanyi hivyo kwa sababu nguo ni nzuri… bali ataonekanaje machoni mwa watu akiwa amevaa nguo hiyo.

4: Nasa Wateja
Ngoja nikunong’oneze SIRI…

Pesa nyingi ziko kwenye orodha ya wateja utakao wanasa!

Kila mwana mwanamasoko/mfanyabishara aliyefanikiwa sana, atakueleza kuwa mafanikio yake yametokana na ukubwa wa wateja alionao katika orodha yake…

Ukiwa na blogu utahitajika kuwa na haya yafuatayo:

Blogu yako iwe na fomu ya kunasa mawasiliano ya wateja kwa ahadi ya kuabdilishana kitu. Mfano, unaweza kuwapa kijitabu kitakacho wafunza na kuwapa mbinu za kuondokana na changamoto zinazowakabili, au
Uwaunganishe na ukurasa (Landing Page/Squeeze Page/ Opt-In Page) uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kunasa mawasilaiano yao. Mfano wa ukurasa huo ni kama huu hapa.

Baada ya kunasa mawasilaiano yao, kazi inayofuata ni ku…

5: Jenga Mahusiano Mema Na Orodha Yako!
Watu hupendelea kununua bidhaa na hata kupata huduma kutoka kwa watu/mtu wanayemwamini na kumpenda. Huwa hawajili sana uzuri wa bidhaa na hata huduma yako. Wanakuangalia wewe. Wanchotaka kujua ni, kupitia wewe matatizo yao yanayowaleta kwako yataisha? Hilo tu!

Hivyo, badala ya kutia mkazo zaidi katika kuwauzia bidhaa na huduma, tilia mkazo zaidi katika kujenga uaminifu. Wakuone u-mjuzi katika kile unachokifanya zaidi kuliko bidhaa yenyewe. Unaweza kufanya hivyo kupitia mfumo wa teknolojia ya kutuma ujumbe inayokupa fursa ya kufanya hivyo kwa mara moja (email marketing software). Yaani, unaandika ujumbe mmoja unautuma kwenda kwa watu wote walioko kwenye orodha yako ukitaja majina yao.

Hakikisha pia katika ujumbe huo, usiwe wa kuwauzia bidhaa badala yake waelimishe. Unajua kitakachotokea baada ya hapo? Si kingine, bali ni….

6: Anza Kuingiza Pesa
Baada ya kujenga mahusiano ya kutosha, sasa unaweza kuanza kutangaza bidhaa zako na uwaeleze watanufaika vipi kwa kutumia huduma na hata bidhaa zako.

Katika hatua hii, kimsingi usiwe mwoga hata kidogo. Yafaa ueleze bidhaa zako ukiwa na hamasa kubwa, mchangamfu, mwenye uhakika bidhaa zako kutoa manufaa halisi wanayokusudia. Hakika watanunua na zaidi watafurahia kupata huduma kutoka kwako.

Hadi hapo naamini umeshajua namna unavyoweza kutumia blogu yako kujenga biashara yako.

BONASI: Hii hapa ni video ya Mike Dillard akieleza alivyotumia njia nilizotaja hapo juu na sasa huweza kutengeneza Dola za kimarekani $705,821.93 kwa wiki moja. Anatumia mfumo wa blogu.

Binafsi ninayo mission…nayo ni kuwasaidia watu wachache walio na shauku ya kujifunza mbinu mpya za kujiajiri kupitia mtandao wa inateneti. Sharti ni moja…uwe na laptop na uwe tayari kutumia angalau masaa mawili kwa siku. Kama unadhani unakidhi vigezo hivyo, basi huna sababu ya kusubiri. Jisajiri na mtandao huu kwa kubofya neno REGISTER hapo juu! Ukishajisajiri, niongeze kwenye orodha yako ya marafiki alafu chini kwenye comment box niandikie azma yako, nami nitakujibu.

Tutaonana muda mfupi ujao!